Genesis 48

Genesis 48:1

Ikawa

Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi.

mmojawapo akamwambia Yusufu

"mtu akamwambia Yusufu"

Tazama, baba yako

"Sikiliza, baba yako". Hapa neno "tazama" linatumika kuvuta nadhari ya Yusufu.

Hivyo akaondoka

"Kwa hiyo Yusufu akaondoka"

Yakobo alipoambiwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mtu alipomuambia Yakobo"

mwanao Yusufu amekuja kukuona

"mwanao Yusufu amekuja kwako"

Israeli akakusanya nguvu na kukaa juu ya kitanda

Hapa mwandishi anazungumzia juu ya Israeli kuhangaika kuketi kitandani kana kwamba alikuwa akikusanya "nguvu" kama vile mtu akusanyavyo vitu halisia. "Israeli alifanya bidii kubwa kukaa kitandani" au "Israeli alihangaika alipokaa juu kitandani"

Genesis 48:3

Luzu

Hili ni jina la mji.

katika nchi ya Kanaani. Akanibariki na kuniambia

Hii inaweza kutafsiriwa kwa sentensi mpya ikianzia katika sehemu mpya. "katika nchi ya Kaanani, na akanibariki. Na akasema kwangu"

akanibariki

Hii ina maana ya Mungu kutamka baraka rasmi kwa mtu.

na kuniambia, 'Tazama, nitakupa uzao mwingi, na kukuzidisha. Nitakufanya kuwa kusanyiko la mataifa. Nitakupa nchi hii wewe na uzao wako kuwa milki ya milele

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "na kusema kwangu ya kwamba angenifanya niwe na uzao mwingi na kunizidishia. Na akasema ya kwamba angenifanya kuwa kusanyiko la mataifa na angenipa nchi hii kwa uzao wangu kama milki ya milele".

Tazama

Mungu alitumia neno hili "tazama" hapa kumuamsha Yakobo kuvuta nadhari kwa kile alichokuwa akitaka kumwambia.

nitakupa uzao mwingi, na kukuzidisha

Msemo "kukuzidishia" unaelezea jinsi ambavyo Mungu angemfanya Yakobo "kupata uzao". "Nitakupatia uzao mwingi sana"

Nitakufanya kuwa kusanyiko la mataifa

Hapa "nitakufanya" ina maana ya Yakobo, lakini ina maana ya uzao wa Yakobo. "Nitafanya vizazi vyako kuwa mataifa mengi"

milki ya milele

"milki ya kudumu"

Genesis 48:5

sasa

Hii haimaanishi "katika kipindi hiki" lakini inatumika kuvuta nadhari kwa lengo muhimu linalofuata.

Efrahimu na Manase watakuwa wangu

Efrahimu na Manase kila mmoja atapokea sehemu ya nchi kama ndugu zake Yusufu.

watahesabiwa katika majina ya ndugu zao katika urithi wao

Maana zinawezekana kuwa 1) watoto wale wengine wa Yusufu wangerithi nchi kama sehemu ya makabila ya Efrahimu na Manase au 2) Yusufu atatengewa nchi na Efraimu na Manase na watoto wengine wa Yusufu watarithi nchi hiyo. "na kwa urithi wao, utawaorodhesha chini ya majina ya ndugu zao"

Efrathi

Hili ni jina lingine la mji wa Bethlehemu.

ndio, Bethlehemu

Mwandishi huyu anatoa taarifa ya nyuma.

Genesis 48:8

Ni nani hawa?

"Hawa ni watoto wa nani?"

niwabariki

Baba huwa anatamka baraka rasmi juu ya watoto au wajukuu wake.

Basi macho ya Israeli ... hakuweza kuona

Neno "Basi" linatumika hapa kuweka alama ya badiliko kutoka kwenye simulizi kwenda kwa taarifa ya nyuma kuhusu Israeli.

akawabusu

"Israeli aliwabusu"

Genesis 48:11

kuuona uso wako tena

Hapa "uso" ina maana ya mtu mzima. "Kukuona mara nyingine"

katikati ya magoti ya Israeli

Yusufu alipowaweka wanawe juu ya mapaja ya Israeli au magotini ilikuwa ishara ya kwamba Israeli alikuwa akiwachukua. Hii iliwapa watoto hawa urithi maalumu kutoka kwa Yakobo.

kisha akainama na uso wake juu ya nchi

Yusufu aliinama chini kuonyesha heshima kwa baba yake.

Manase katika mkono wake wa kulia kuelekea mkono wa kulia wa Israeli

Yusufu anawaweka wavulana ili kwamba Israeli aweze kuweka mkono wake wa kuume juu ya Manase. Manase alikuwa ndugu mkubwa na mkono wa kulia ilikuwa ishara ya kwamba angepokea baraka kubwa.

Genesis 48:14

mkono wake wa kulia na kuuweka juu ya kichwa cha Efrahimu

Kuweka mkono wa kulia juu ya kichwa cha Efraimu ilikuwa ishara ya kwamba angepokea baraka kubwa.

Israeli akambariki Yusufu

Hapa "Yusufu" pia ina maana ya Efraimu na Manase. Kwa kuwa Yusufu ni baba, ni yeye pekee anayetajwa hapa.

Mungu ambaye mbele zake baba zangu Ibrahimu na Isaka walitembea

Kumtumikia Mungu inazungumziwa kana kwamba ilikuwa kutembea mbele za Mungu. "Mungu ambaye babu yangu Abrahamu na baba yangu Isaka alimtumikia"

aliyenitunza

Mungu alimtunza Israeli kama vile mfugaji anavyotunza kondoo wake. "ambaye alinitunza kama mfugaji atunzavyo wanyama wake"

malaika

Maana zinawezekana kuwa 1) hii ina maana ya malaika ambaye Mungu alimtuma kumlinda Yakobo au 2) hii ina maana ya Mungu aliyemtokea kama malaika kumlinda Yakobo.

aliyenilinda

"aliniokoa"

Jina langu na litajwe kwao, na majina ya baba zangu Abrahamu na Isaka

Hapa "jina" lina maana ya mtu mzima. Msemo "jina langu na litajwe kwao" ni lahaja ambayo ina maana ya kwamba mtu anakumbukwa kwa sababu ya mtu mwingine. Hii inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. "Watu wamkumbuke Abrahamu, Isaka, na mimi kwa sababu ya Efraimu na Manase"

Na wawe makutano ya watu juu ya nchi

Hapa "wawe" ina maana ya Efraimu na Manase, lakini ina maana ya uzao wao. "Na wawe na uzao mwingi ambao utaishi ulimwenguni kote"

Genesis 48:17

ameweka mkono wake wa kulia juu ya kichwa

Mkono wa kulia ulikuwa ishara ya baraka kubwa ambayo mwana mkubwa alitakiwa kupokea.

Genesis 48:19

Yeye naye atakuwa watu, naye pia atakuwa mkuu

Hapa "yeye" ina maana ya Manase, lakini inahusu uzao wake. "Mwana wako mkubwa atakuwa na uzao mwingi, nao watakuja kuwa taifa kubwa"

siku hiyo kwa maneno haya

Hapa "maneno" ina maana ya kile kilichosemwa. "siku hiyo, akisema"

Watu wa Israeli watatamka baraka kwa majina yenu wakisema

"Watu wa Israeli watazungumza majina yenu pale wanapowabariki wengine"

kwa majina yenu wakisema, Mungu na akufanye kama Efrahimu na kama Manase

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "kwa majina yenu. Watamuuliza Mungu kuwafanya wengine kama Efraimu na kama Manase"

kama Efrahimu na kama Manase

Israeli kusema jina la Efraimu kwanza ni njia nyingine anaonyesha ya kwamba Efraimu atakuwa mkubwa kuliko Manase.

Israeli akamweka Efrahimu mbele ya Manase

Kumpatia Efraimu baraka kubwa na kumfanya awe wa muhimu kuliko Manase inazungumziwa kana kwamba Israeli amemuweka kihalisia wa mwili Efraimu mbele ya Manase.

Genesis 48:21

atakuwa nanyi ... atawarudisha ... baba zenu

Hapa "nanyi" na "zenu" ni wingi na ina maana ya watu wote wa Israeli.

atakuwa nanyi

Hii ni lahaja yenye maana ya Mungu atasaidia na kubariki watu wa Israeli. "Mungu atakusaidia" au "Mungu atakubariki"

atawarudisha

Hapa "atawarudisha" inaweza kutafsiriwa kama "kuchukua"

nchi ya baba zenu

"nchi ya mababu zenu"

Kwako wewe, kwa kuwa uko juu ya ndugu zako, ninakupa mtelemko wa mlima

Maana zinawezekana kuwa 1) Yusufu kuwa na heshima na mamlaka zaidi kuliko ndugu zake inazungumziwa kana kwamba alikuwa juu yao kiuhalisia wa kimwili. "Kwako, ambaye ni mkubwa kuliko ndugu zako, ninakupa mteremko wa mlima" au 2) Yakobo ana maanisha anatoa nchi zaidi kwa Yusufu kuliko anavyotoa kwa ndugu wa Yusufu. "Kwako, ninakupa kilima kimoja zaidi ya nayowapatia ndugu zako. Ninakupatia mteremko wa mlima"

Kwako wewe

Hapa "wewe" ni umoja na ina maana ya Yusufu.

mteremko wa mlima niliouchukuwa kutoka kwa Waamori kwa upanga wangu na upinde wangu

Hapa "upanga" na "upinde" ina maana ya kupigana vitani. "sehemu ya nchi niliyopigania na kuchukua kutoka kwa Waamori"