Genesis 49

Genesis 49:1

Maelezo ya Jumla:

Hii inaanza baraka za mwisho za Yakobo kwa wanawe. Hii inaendelea hadi 49:27. Baraka za Yakobo zinaandikwa kwa namna ya shairi.

Kusanyikeni ninyi wenyewe na msikilize, enyi wana wa Yakobo. Msikilizeni Israeli, baba yenu

Sentensi mbili zinasema jambo moja kuweka msisitizo. "Njooni na msikilize kwa makini baba yenu"

wana wa Yakobo. Msikilizeni Israeli, baba yenu.

Yakobo anajitambua katika lugha ya mtu wa utatu. Inaweza kusemwa katika lugha ya mtu wa kwanza. "wanangu. Nisikilizeni, baba yenu"

Genesis 49:3

mzaliwa wangu wa kwanza, nguvu zangu, na mwanzo wa uwezo wangu

Misemo ya "mzaliwa wangu wa kwanza, nguvu zangu" na "mwanzo wa uwezo wangu" zina maana moja. Maneno "uwezo" na "nguvu" yana maana ya uwezo wa Yakobo kuzaa watoto. Maneno "mzaliwa wa kwanza" na "mwanzo" ina maana ya kwamba Rubeni ni mwanawe wa kwanza. "mwanangu wa kwanza nilipokuwa mwanamume"

aliyesalia katika heshima na nguvu

Hii inaweza kuwekwa kama sentensi mpya. "Wewe ni wa kwanza kwa heshima na nguvu" au "Unawapita wengine wote kwa heshima na nguvu"

Asiyezuilika kama maji yarukayo

Yakobo anamlinganisha Rubeni na maji yenye mkondo mwenye nguvu kusisitiza ya kwamba hawezi kujizuia hasirayake na hayupo imara.

hautakuwa na umaharufu

"hautakuwa wa kwanza miongoni mwa ndugu zako"

kwa sababu ulikwenda juu ya kitanda cha baba yako. Hata ukakitia unajisi; ulipanda juu ya kitanda changu

Hapa "kitanda" na "juu ya kitanda changu" ina maana ya suria wa Yakobo, Bilha. Yakobo ana maanisha pale ambapo Rubeni alilala na Bilha. "kwa sababu ulipanda kitandani mwangu na kulala na Bilha suria wangu. Umeniaibisha"

ulikwenda juu ya kitanda cha baba yako ... ulipanda juu ya kitanda changu

Kaluli zote mbili zina maana moja.

Genesis 49:5

Simoni na Lawi ni ndugu

Hii haimaanishi tu ya kwamba wao ni ndugu kwa kuzaliwa. yakobo anasisitiza ya kwamba walishirikiana pamoja kuwaua watu wa Shekemu.

Panga zao ni silaha za vurugu

"Wanatumia panga zao kudhuru na kuua watu"

Ee nafsi yangu ... moyo wangu

Yakobo anatumia maneno "nafsi" na "moyo" kujitambulisha na kusema ya kwamba watu wengine, na labda Mungu pia, wanamheshimu sana ya kwamba hatamani kujiunga na wale wanaopanga kufanya uovu.

usiingie barazani pao; usiingie katika mikutano yao

Misemo hii miwili ina maana moja. Yakobo anaunganisha kuweka msisitizo ya kwamba hataki kushirikiana katika mipango yao miovu. "hakika sitajiunga nao kufanya mipango yoyote"

kuwakata visigino ng'ombe.

Hii ina maana ya Simoni na Lawi kulemaza ng'ombe kwa starehe tu.

kuwakata visigino

Hii ina maana ya kukata visigino vya miguu ya wanyama ili isiweze kutembea.

Genesis 49:7

Hasira yao na ilaaniwe, kwani ilikuwa kali - na ukali wao, kwani ulikuwa ni katili

Mungu kumlaani Simoni na Lawi inazungumziwa kana kwamba Mungu alikuwa akilaani hasira na ukali wao. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Bwana anasema, 'Nitawalaani kwa sababu ya hasira yao kali na ukali wao mkatili" au "Mimi, Bwana, nitawalaani kwa sababu ya hasira ya kali na ukali wao mkatili"

Hasira yao na ilaaniwe

Katika unabii, nabii mara nyingi huzungumza maneno ya Mungu kana kwamba Mungu mwenyenwe alikuwa akizungumza. Hii inasisitiza ukaribu ulivyo kati ya nabii na Mungu.

na ukali wao, kwani ulikuwa ni katili

Neno "nitalaani" linaeleweka. "nami nitalaani ukali wao, maana ulikuwa katili"

Nitawagawa katika Yakobo na kuwatawanya katika Israeli

Neno "Nitawagawa" lina maana ya Mungu. Neno "kuwatawanya" lina maana ya Simoni na Lawi lakini ni lugha nyingine yenye maana ya uzao wao. Maneno "Yakobo" na "Israeli" ni lugha nyingine yenye maana ya watu wote wa Israeli. "Nitawagawanya uzao wao na kuwasambaza miongoni mwa watu wote wa Israeli"

Genesis 49:8

ndugu zako watakusifu ... Wana wa baba yako watainama mbele zako

Kauli hizi mbili zina maana moja.

watakusifu. Mkono wako

Sentensi ya pili inaeleza sababu ya sentensi ya kwanza. Neno "kwa" au "kwa sababu" linaweza kuongezwa kuweka hii wazi. "nitakusifu wewe. Kwa mkono wako" au "nitakusifu kwa sababu mkono wako"

Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako

Hii ni njia ya kusema. "Utawashinda adui zako"

watainama

Hii ina maana kuinama kwa unyenyekevu kuonyesha heshima na taadhima kwa mtu.

Genesis 49:9

Yuda ni mwana simba

Yakobo anamzungumzia Yuda kana kwamba alikuwa mtoto wa simba. Yakobo anasisitiza nguvu ya Yuda. "Yuda ni kama mwana wa simba"

Mwanangu, umetoka katika mawindo yako

"Wewe, mwanangu, umerudi kutoka kula windo lako"

kama simba jike

Yakobo anamlinganisha Yuda na simba jike. Simba jike ni mwindaji na mlinzi wa msingi wa watoto wake.

Je nani atakayejaribu kumwamsha?

Yakobo anatumia swali kusisitiza jinsi Yuda anavyotisha watu wengine. "Hakuna atakaye kumuamsha"

Genesis 49:10

Fimbo haitaondoka katika Yuda, wala fimbo ya utawala kutoka katika miguu yake

"Fimbo" na "fimbo ya utawala" ni miti iliyopambwa ambayo wafalme hubeba. Hapa ni lugha nyingine yenye maana ya nguvu ya utawala. Na "Yuda" ina maana ya uzao wake. "Nguvu ya kutawala daima itakuwa ndani ya uzao wa Yuda"

hata atakapo kuja Shilo. Mataifa yatamtii

Maana zawezekana kuwa 1) "Shilo" ina maana "shukrani". "hadi pale mataifa yatamtii na kuleta shukrani kwake" au 2) "Shilo" ina maana ya mji wa Shilo. "hadi pale mtawala atakuja Shilo. Kisha mataifa yatamtii." Watu wengi huchukulia hili kama unabii kuhusu Mesia ambaye ni uzao wa Mflame Daudi. Daudi ni uzao wa Yuda.

Mataifa yatamtii

Hapa "mataifa" ina maana ya watu. "Watu wa mataifa watamtii"

Genesis 49:11

Kumfunga punda wake ... katika mzabibu mzuri

Kauli zote mbili zina maana moja. Inasemekana ya kwamba mizabibu imejaa zabibu ambayo bwana hajali kama punda inavila baadhi yao.

wake ... amefua

Maana za muonakano wa "wake" au "amefua" ni 1) ina maana ya uzao wa Yuda. "wake ... wame" au 2) ina maana ya mtawala katika 49:10, ambayo inaweza kumaanisha Mesia.

amefua ... katika damu ya vichala vya mzabibu

Kauli zote mbili zina maana moja. Inasemekana ya kwamba kuna zabibu nyingi sana hadi wanaweza kufua nguo zao kwa maji yake.

amefua

Mara nyingi katika unabii matukio yatakoyotokea hapo baadae yanaelezwa kama jambo lililokwisha tokea zamani. Hii inasisitiza ya kwamba tukio hili hakika litatokea. "watafua" au "atafua"

damu ya vichala vya mzabibu

HIi inazungumzia kuhusu maji ya zabibu kana kwamba yalikuwa damu. Hii inasisitiza jinsi gani maji yalikuwa mekundu.

Macho yake yatakuwa meusi kama mvinyo

Hii ina maana ya rangi ya macho ya mtu kulinganisha na rangi ya mvinyo mwekundu. Maana zaweza kuwa 1) macho meusi ina maana macho yenye afya au 2) macho ya watu yatakuwa mekundu kutokana na kunywa mvinyo mwingi

meno yake meupe kama maziwa

Hii inalinganisha rangi ya meno ya watu kwa weupe wa rangi ya maziwa. Hii inasemekana ya kwamba kutakuwa na ng'ombe wengi wenye afya na kuwa na maziwa mengi ya kunywa.

Genesis 49:13

Zabuloni atakaa

Hii ina maana ya uzao wa Zabuloni.

Atakuwa bandari

Hapa "atakuwa" ina maana ya miji ya baharini ambayo watu wa Zabuloni wataishi au kujenga. Miji hii itatoa hifadhi kwa meli.

bandari

sehemu ya bahari ambayo ipo karibu na nchi na ipo salama kwa ajili ya meli.

Genesis 49:14

Isakari ni punda mwenye nguvu

Yakobo anazungumzia kuhusu Isakari na uzao wake kana kwamba walikuwa punda. Hii inasisitiza ya kwamba watafanya kazi kwa bidii. "Uzao wa Isakari utakuwa kama punda mwenye nguvu"

Isakari ni

Mara nyingi katika unabii matukio ambayo yatatokea baadae inaelezwa kama kitu ambacho tayari kinaendelea. Hii inasisitiza ya kwamba tukio litatokea hakika. Inaweza kuwekwa kwa lugha ya baade. "Isakari atakuwa" au "Uzao wa Isakari utakuwa"

Isakari ... Anaona ... Atainamisha

Hapa "Isakari" ni lugha nyingine yenye maana ya uzao wake. "Uzao wa Isakari ... Wanaona .. Wataona"

ajilazaye kati ya kondoo

Maana zaweza kuwa 1) "ajilazaye chini katikati ya kundi walizokuwa wakibeba" au 2) "ajilazaye chini katikati ya zizi la kondoo".Kwa namna yoyote ile, Yakobo anazungumzia kuhusu uzao wa Isakari kana kwamba walikuwa punda ambao wamefanya kazi kwa bidii na wamejilaza chini kupumzika.

mahali pazuri pa kupumzikia na nchi ya kupendeza

"sehemu ya kupumzikia ambayo ni nzuri na kwamba nchi inapendeza"

Atainamisha bega lake kwa mzigo

Msemo huu "Atainamisha bega lake kwa mzigo" ni njia ya kusema "fanya kazi kwa bidii kubeba mzigo"

kuwa mtumishi wake kwa kazi ile

"watafanya kazi kwa wengine kama watumwa"

Genesis 49:16

Dani atawaamua watu wake

Hapa "Dani" ina maana ya uzao wake. "Uzao wa Dani utawaamua watu wake"

watu wake

Maana zinazowezekana za "watu wake" ni 1) "watu wa Dani" au 2) "watu wa Israeli"

Dani atakuwa nyoka kando ya njia

Yakobo anazungumza kuhusu Dani na uzao wake kana kwamba walikuwa nyoka. Ingawa nyoka ni mdogo, inaweza kumshusha aongozaye farasi chini ya farasi wake. Kwa hiyo Dani, ingawa kabila dogo, ni la kutisha sana kwa adui zake. "Uzao wa Dani utakuwa kama nyoka kando ya barabara"

Ninaungoja wokovu wako, Yahwe.

Nomino inayojitegemea "wokovu" inaweza kutafsiriwa kama "kuokoa". "Ninakusubiri, Yahwe, kunikoa"

Ninaungoja

Neno "Ninaungoja" ina maana ya Yakobo.

Genesis 49:19

Gadi ... Asheri ... Naftali

Hawa ina maana ya vizazi vya kila mwanamume.

katika visigino vyao

Hapa "visigino" ina maana ya wavamizi ambao wanatoroka kutoka kwa uzao wa Gadi.

Vyakula vitakuwa vingi

Hapa "vingi" ni njia ya kusema "vitamu"

Naftali ni dubu jike asiyefungwa

Yakobo anazungumzia kuhuus uzao wa Naftali kana kwamba walikuwa paa wa kike ambaye yupo huru kukimbia. Hii inaweza kusisitiza ya kwamba watakuwa wajumbe wepesi. "Uzao wa Naftali utakuwa kama paa aliyeachiwa huru"

atakuwa na watoto wa dubu walio wazuri

"mtoto wa paa". Maana kwa lugha ya Kihebrania haipo wazi. Baadhi ya tafsiri hutafsiri kama "ana maneno mazuri" au "kuzungumza mambo mazuri"

Genesis 49:22

Yusufu ni tawi lizaalo

Hapa "Yusufu" ni lugha nyingine yenye maana ya uzao wake. Yakobo anazungumzia uzao kana kwamba walikuwa shina la mti lizaalo matunda mengi. Hii inasisitiza ya kwamba wataongezeka sana kwa idadi.

tawi

shina kuu la mti

ambaye matawi yake yako juu wa ukuta

Shina ambalo litakuwa na kusambaajuu ya ukuta inazungumziwa kana kwamba ilikuwa inapanda.

Genesis 49:24

Maelezo ya Jumla:

Yakobo anaendelea kumbariki Yusufu na uzao wake.

upinde wake utakuwa imara

Mtu anayeshikilia upinde kwa umakini inazungumziwa kana kwamba uoinde mwenyewe utakuwa imara. Inasemekana anaushikilia kwa ustadi anapopima kwa adui wake. "ataushika upinde wake kwa uimara anapolenga adui wake"

upinde wake ... mikono yake

Hapa "wake" ina maana ya Yakobo anayesimama badala ya uzao wake. "upinde wake .. mikono yake"

mikono yake itakuwa hodari

Hapa "mikono" ina maana ya mikono ya mtu anaposhikilia upinde wake kwa makini. "mikono yake utabaki imara anapolenga upinde wake"

mikono ya Mwenye nguvu

"mikono" inaelezea nguvu ya Yahwe. "nguvu ya Mwenye Nguvu"

kwa ajili ya jina la Mchungaji

Hapa "jina" lina maana ya mtu mzima. "kwa sababu ya Mchungaji"

Mchungaji

Yakobo anamzungumzia Yahwe kana kwamba alikuwa "mchungaji". Hii inasisitiza ya kwamba Yahwe anawaongoza na kuwalinda watu wake.

Mwamba

Yakobo anazungumzia kuhusu Yahwe kana kwamba alikuwa "Mwamba" ambao watu wanaweza kuupanda kutafuta usalama kutoka kwa maadui. Hii inasisitiza ya kwamba Yahwe hulinda watu wake.

Genesis 49:25

Maelezo ya Jumla:

Yakobo anaendelea kumbariki Yusufu na uzao wake.

atakusaidia ... atakubariki

Hapa "atakusaidia" ina maana ya Yusufu inayomaanisha uzao wake. "saidia uzao wako ... wabariki"

baraka za mbinguni juu

Hapa "mbinguni juu" ina maana ya mvua ambayo husaidia mazao kuota.

baraka za vilindi vilivyo chini

Hapa "chini" ina maana ya maji chini ya ardhi ambayo hutosheleza mito na visima.

baraka za maziwa na tumbo

Hapa "maziwa na tumbo" ina maana ya uwezo wa mama kupata watoto na kuwanyonyesha maziwa.

Genesis 49:26

Maelezo ya Jumla

Yakobo anaendelea kumbariki Yusufu na uzao wake.

milima ya zamani

Maana ya lugha asili haipo wazi. Baadhi ya tafsiri za Biblia zina "mababu zangu" badala ya "milima ya zamani"

Na viwe katika kichwa cha Yusufu

Hapa "viwe" ina maana ya baraka za baba yake.

juu ya taji ya kifalme kichwani pa ndugu zake

Yakobo anatamani kwa baraka hizi kupitishwa hata kwa wale wazawa muhimu. "juu ya kichwa cha mzawa muhimu wa Yusufu"

mwana wa mfalme kwa ndugu zake

"mtu muhimu wa ndugu zake"

Genesis 49:27

Benjamini ni mbwamwitu mwenye njaa

Hapa "Benyamini" ni lugha nyingine ya uzao. Yakobo anazungumzia juu ya uzao wa Benyamini kana kwamba ulikuwa mbwa mwitu wenye njaa. Hii inasisitiza ya kwamba watakuwa wapiganaji hodari. "Uzao wa Benyamini watakuwa kama mbwa mwitu"

Genesis 49:28

Haya ni makabila kumi na mbili ya Israeli

"Haya" ina maana ya wana wa Yakobo waliotajwa katika 49:1-27. Kila mwana alikuwa kiongozi wa kabila lake mwenyewe.

alipowabariki

Hapa neno "alipowabariki" lina maana ya kuongelea baraka rasmi.

kila mmoja kwa baraka iliyomstahili

"Akawapa kila mtoto baraka inayomstahili"

akawaelekeza

"akawaamuru"

Ninakaribia kwenda kwa watu wangu

Hii ni njia ya upole ya kusema ya kwamba amekaribia kufa. "Nimekaribia kufa"

kwenda kwa watu wangu

Yakobo ana maanisha pale ambapo nafsi yake utakwenda atakapokufa. Anategemea kuwaunga Abrahamu na Isaka katika maisha ya baadae.

Efroni Mhiti

Hili ni jina la mwanamume. "Mhiti" ina maana ya "uzao wa Hethi".

Makpela

Makpela lilikuwa jina la eneo au mahali.

Mamre

Hili lilikuwa jina lingine la mji wa Hebroni. Inawezekana lilitajwa baada ya Mamre, rafiki wa Abrahamu aliyeishi kule.

Genesis 49:31

Maelezo ya Jumla:

Yakobo anaendelea kuzungumza na wanawe.

lililomo lilinunuliwa

Ununuzi unaweza kuwekwa wazi. "ndani mwake ulinunuliwa na Abrahamu"

kutoka kwa watu wa Hethi

"kutoka kwa Wahiti"

alipomaliza maagizo hayo kwa wanawe

"alimaliza kuwaagiza wanawe" au "alimaliza kuwaamuru wanawe"

akaiweka miguu yake kitandani

Yakobo alikuwa amekaa juu ya kitanda. Sasa, Yakobo anageuka na kuweka miguu yake kitandani ili aweze kulala chini.

akavuta pumzi ya mwisho

Hii ni njia ya upole ya kusema mtu amekufa.

akawaendea watu wake

Baada ya Yakobo kufa, nafsi yake ilikwenda sehemu ile ile kama ndugu zake waliokufa kabla yake.