Genesis 15

Genesis 15:1

Baada ya mambo haya

"Mambo haya" ina maana ya pale ambapo wafalme walipigana na Abramu akamuokoa Lutu.

neno la Yahwe likamjia

Lahaja hii ina maana ya Yahwe akazungumza. "Yahwe alizunguza ujumbe wake"

neno la Yahwe

Hapa "neno" inawakilisha ujumbe wa Yahwe. "ujumbe wa Yahwe"

ngao ... thawabu

Mungu alitumia sitiari hizi mbili kumwambia Abramu juu ya tabia yake na uhusiano wake na Abramu.

mimi ni ngao yako

Wanajeshi hutumia ngao kujilinda kwa maadui zao. "Nitakulinda kama ngao" au "Mimi ni ngao yako kukulinda"

thawabu

"malipo". Hii ina maana ya malipo yanayostahili kwa mtu. Maana mbili zaweza kuwa 1) "Mimi ni yote unayohitaji" au 2) "Nitakupa yote unayohitaji".

Abram akasema, "Kwakuwa hujanipatia

"Abramu aliendelea kuzungumza na kusema, "Kwa kuwa umenipatia"

Genesis 15:4

Kisha, tazama

Neno "tazama" linasisitiza ukweli ya kwamba neno la Yahwe lilikuja kwa Abrahamu tena.

neno la Yahwe likaja

Lugha hii ina maana ya kuwa Mungu alizungumza. "Yahwe alizungumza ujumbe wake"

neno la Yahwe

Hapa "neno" linawakilisha ujumbe wa Yahwe. "Ujumbe wa Yahwe"

Mtu huyu

Hii ina maana ya Eliezeri wa Dameski.

atakaye toka katika mwili wako ndiye

"yule utakayekuwa baba yake" au "mwana wako kabisa". Mwana wa Abramu atakuwa mrithi wake.

uzihesabu nyota

"hesabu nyota"

ndivyo uzao wako utakavyokuwa

Kama vile Abramu atavyoshindwa kuhesabu nyota zote, hataweza kuhesabu uzao wake wote kwa sababu utakuwa mwingi sana.

Genesis 15:6

Akamwamini Yahwe

Hii ina maana alipokea na kuamini kile Yahwe alichosema ni kweli.

akamuhesabia jambo hili kuwa mwenye haki

"Yahwe alimhesabia imani ya Abramu kama haki" au "Yahwe alimchukulia Abramu kuwa na haki kwa sababu Abramu alimuamini"

Mimi ni Yahwe, niliye kutoa katika Uru

Yahwe alikuwa akimkumbusha Abrahamu kile alichokuwa amefanya ili Abrahamu aweze kumjua Yahwe alikuwa na nguvu kumpatia Abramu kile alichomuahidi.

kuirithi

"kukipokea" au "ili kwamba ukimiliki"

nitajua je

Abramu alikuwa akiulizia ushahidi zaidi ya kwamba Yahwe atampatia ile nchi.

Genesis 15:9

mizoga

"miili iliyokufa ya wanyama na ndege"

Abram akawafukuza

"Abramu aliwafukuza ndege". Alihakikisha ndege hawakula wanyama waliokufa.

Genesis 15:12

Abramu akalala usingizi

Hii ni lahaja. "Abrahamu alilala usingizi mzito"

giza zito na la kutisha

"giza kubwa sana lililomtisha"

ikamfunika

"ikamzunguka"

wageni

"wageni"

watatumikishwa na kuteswa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "na wamiliki wa nchi ile watawatumikisha na kuwatesa"

Genesis 15:14

Taarifa ya Jumla:

Yahwe aliendelea kuzungumza na Abramu wakati Abramu alipokuwa akiota.

Nitahukumu

Hapa "hukumu" ni lugha nyingine kwa kile kitakachotokea baada ya Mungu kutoa hukumu. "Nitaadhibu"

wataowatumikia

Maana kamili ya kauli hii inawezwa kufanywa wazi. "ambao vizazi vyako watawatumikia"

mali nyingi

Hii ni lahaja. "mali nyingi" au "utajiri mkubwa"

utakwenda kwa baba zako

Hii ni njia ya upole ya kusema "utakufa"

baba

Neno "baba" lina maana sawa na mababu. "mababu"

utazikwa katika uzee mwema

"utakuwa mzee sana utakapokufa na familia yako itazika mwili wako"

Katika kizazi cha nne

Hapa kizazi kimoja kina maana ya urefu wa miaka 100. "Baada ya miaka mia nne"

watakuja tena hapa

"vizazi vyako watakuja hapa tena". Vizazi vya Abrahamu vitakuja katika nchi ampabo Abramu alikuwa akiishi, nchi ambayo Yahwe aliahidi kumpatia.

haujafikia mwisho wake

"haijakamilika" au "itakuwa mbaya zaidi kabla sijawaadhibu"

Genesis 15:17

tazama

Neno "tazama" hapa linatuamsha kuwa makini kwa taarifa ya kushangaza inayofuata.

moshi wenye moto na miali ya mwanga ilipita kati ya vile vipande

Mungu alifanya hivi kumuonyesha Abramu ya kuwa alikuwa akifanya agano na yeye.

ilipita kati ya vile vipande

"ilipita katikati ya mistari miwili ya vipande vya wanyama"

agano

Katika agano hili Mungu alimuahidi kumbariki Abramu, naye ataendelea kumbariki ikiwa Abramu ataendelea kumfuata yeye.

Ninatoa nchi hii

Kwa kusema hivi, Mungu alikuwa akiwapa uzao wa Abramu nchi. Mungu alikuwa akifanya hivi, lakini uzao hawakuweza kwenda katika nchi hadi baada ya miaka mingi baadae.

mto mkuu, Frati

"mto mkubwa, Frati". Hizi ni njia mbili zinazoelezea mto mmoja.

Mkeni , Mkenizi, na Mkadmoni, Mhiti, Mperizi, Mrefai, Mwamori, Mkanaani, Mgirgashi, na Myebusi.

Haya ni majina ya makundi ya watu ambao waliishi katika nchi. Mungu angeruhusu uzao wa Abrahamu kuwashinda watu hawa na kuchukua nchi yao.