sura 7

1 Ni namna yani miundi yako yeivyo yaonekana ni mitana mwe viatu, mwana kivyee ywa mfaume,! Nyonga yako nikana mkufu, kana ndima ya wazengao. 2 Ukuvu wakoni kana duala sabakui hata deseku kosa mhanganyiko wa mvinyo. Ifu dako ni kana ngano yekuumuka yo na kuzunguusiwa nyinyolo. 3 Matombo yako maidi ni kana wana waidi waayala mapacha na yala. 4 Singo yako ni kana mnaa wa npembe,meso yako ni kana ma ziwa ya Heshiboni mwe lango la Bathi "Rabim. Npua yaako ni kana mnaa wa Lebanoni ambao wakauwa Damasko. 5 Mutwi wako ni kana Kaemeli, fii mwe mutwi wako ni za zahabu size, Mfaume kastaajabishwa ni vifundo vyakwe vya fii. Ni 6 namna yani weivyomtana na kuagozwa, mpenzi na matana yako. 7 Uwe wako ni kana mti wa mtende, na matombo yako ni ka na vifungu vya matunda. 8 Matombo yako na yawe kana vifungu vya mizabibu na halufu ya npua yako ni kana mapea. 9 Muomo wako na uwe kana mvinyo bola, ukaseeya npaahoe kwa mpenzi ywangu. Ukateeya mwe miomo yetu na meno Mvyee mdodo atamwiia mwenye. 10 Mimi ni ywa mpenzi ywnagu na a'ntamani. Soo 11 mpenzi ywangu, tite chongoi ya mzi, tigone nakiyo mwe vijiji. 12 Tenuke mapema tite kwe minda ya mizabibu, tione kana mizabibu isitawi kana isuka na kana mikomamanga iavya maua. Hada nenda nikwenke penzi dangu. 13 Mitunguja yaavya halufu yakwe; mwe uvi wa tekaaho kuna mbaiya matunda mahya na yakae nikuwayo nkikuhi fadhia mpenzi ywangu.